Jinsi ya kubadilisha wazo lako la biashara kuwa biashara kamili: kutengeneza mpango wa biashara.

Kama utakavyojifunza, kuandika mpango wa biashara ni kujumlisha juhudi na utafiti wote uliofanya mpaka sasa. Mchakato wa kuandika mpango wa biashara utakusaidia kuelewa biashara yako na ni nini ufanye ili uweze kuifanikisha. Kutegemeana na biashara yako, mpango wako unaweza kuwa fupi, ukitumia bullet points, au inaweza kuwa ndefu, kama ripoti. Cha muhimu, inakupa wewe, au yeyote mwenye maslahi ya biashara yako, ubayana wavvipengele vyote vya biashara yako.