Ukuaji wa jinsi ya kufikiria ni namna ya kuangalia dunia na mazingira yako kwa namna ya kuona fursa. Kuwa na ukuaji katika kufikiri ni jinsi ya kuchukua fursa mbalimbali. Watu wengine wana ukuaji katika namna ya kufikiri ila kwa watu wengine inabidi wafanye mazoezi ili kuwa hivyo.

Hizi ni sheria ambazo zinaweza kukusaidia kwenye ukuwaji wa kufikiria:

  1. Unaweza jifunza kutoka kwa watu wengi zaidi na sehemu nyingi kuliko unavyodhani.Unatakiwa ufungue macho na kutazama yanayotokea duniani.
  1. Ni muhimu kujifunza kila ujuzi. Mtu aliyepevuka uwezo wa kufikiri atataka kujifunza ujuzi wowote hata kama hana mpango wa kuutumia.
  1. Upevukaji wa mawazo inamaanisha kuchukua fursa zote zinazotokea. Kubali kwenda kwenye shughuli yoyote, kikao au mkusanyiko ambao utakupa nafasi ya kukutana na watu wapya.
  1. Usikae useme “Nimeshindwa” sema “Sijafanikiwa bado”. Ni sawa kujiona mjinga unapoanza kujifunza. Ni kawaida na si rahisi kujifunza ujuzi mpya. Na unaweza patwa na uoga.
  1. Kuwa tayari kujitolea muda wako kujifunza. Ikimaanisha unaweza kuwa unajitolea, au kufanya kazi bila malipo au kukesha usiku ukisoma. Kama unataka kujifunza jinsi ya kushona magauni inamaanisha inabidi ufanye kazi bure kwa fundi wa kushona magauni.
  1. Upevukaji wa mawazo inaaanisha zaidi ya chochote, maisha yako ya zamani hayana uhusiano na maisha yako ya baadaye.

Unaweza kujifunza mengi zaidi kwa angalia video yetu ya Ongeza Ujuzi Wako. Fuatilia kurasa yetu ya Facebook kujifunza mengi zaidi.