Kutathmini wazo la biashara kwa kuboresha na kupima bidhaa au huduma yako.

Unaweza kushangazwa kwamba, kwa kutumia bidii na ubunifu, unaweza kutengeneza sampuli ya bidhaa au huduma yako na kuipima kupitia wateja wako walengwa. Iwapo unatoa mafunzo ya dansi au unafungua mama lishe, ipo njia ya kupima bidhaa au huduma yako. Kuwa tayari kukosolewa, na utumie hayo maoni kuboresha wazo lako kisha, lipime tena!