Jinsi ya kujenga wazo bora la biashara.

Wajasiriamali hodari huwa makini na wenye mtazamo chanya. Katika somo hili tutakufundisha jinsi ya kuchunguza mazingira yako ya karibu ili upate mawazo ya kibiashara yatakayokuletea kipato. Tatizo au hitaji lolote linaloweza kubadilishwa kuwa bidhaa au huduma ambayo watu wanaihitaji, linaweza kuwa wazo la biashara!