Kuanzisha Biashara Somo la 1: Jinsi ya kujenga/kupata wazo la biashara linalokufaa kwa kuchunguza rasilimali zako za ndani.

Wajasiriamali hodari huwa wanaanza na mawazo mazuri. Mafanikio ya kibiashara sio bahati, yanahitaji uvumulivu na bidii. Mchakato wa kutengeneza wazo la biashara si tofauti. Katika somo hili, tutakufundisha jinsi ya kutumia vitu au mambo unayoyapenda, ujuzi na tabia na misimamo yako kutengeneza mawazo ya biashara yatakoyokuletea kipato. Kumbuka, wazo la mtu mmoja si lazima limfae mtu mwingine.