Kati ya vitu vigumu sana ni pamoja na kupata ajira iwe kwenye kampuni, taasisi, au hata kuajiriwa na mtu binafsi. Kutafuta kazi ni shughuli pevu sana. Fungua kurasa za matangazo ya kazi kwenye magazeti au majarida na utaona ninachokusudia! Kila kazi inahitaji uzoefu! Swali linalokuja ni je, utapataje ajira kama huna uzoefu? Hizi ni kanuni 6 ambazo zinaweza kukusaidia.

Kanuni 1: KUPATA KAZI NDIO KAZI YENYEWE!
Inahitaji juhudi kubwa. Hakuna ANAYEKUPA kazi. Ni lazima UISOTEE/UIHANGAIKIE

Kanunu 2: DADISI JE KAZI HIYO INAHUSU NINI
Tayarisha orodha ya wale wote unaowafahamu, uone nani anaweza kukusaidia. Tafuta kiWANGO cha kuingia kwenye hiyo kazi. Usiombe chochote zaidi ya kiwango cha hiyo mkazi. Hili ni kosa kubwa linalofanywa na wengi. Usiombe kuwa meneja miradi ikiwa hujawahi kusimamia mradi wowote hapo kabla!

Kanuni 3: NIA YA CV NI KUKUFANYA TU UITWE KWENYE USAILI
Orodhesha mambo yako muhimu ya kweli unayodhani yatakufanya wewe ni mtaji mzuri. Tafuta njia ya kuunganisha hisia na uzoefu wa maisha yako kwenye hiyo kampuni, kisha ueleze jinsi gani hali hiyo inavyoweza kukufanya uwajibike pale utakapoajiriwa.

Kanuni 4: USIONGOPE/USIDANGANYE
Utabambwa wakati wa mahojiano na utaondoshwa mara moja. Baada ya jina na anuani yako, jiulize – kwa nini mimi ni mtu sahihi kwa kazi hiyo wakati sina ujuzi wowote? LAZIMA ujibu swali hilo kwa uaminifu. Kama huwezi basi unaomba kazi ambayo si sahihi.

Kanuni 5: SAHIHISHA
Makosa kwenye CV yanamweleza msomaji kuwa wewe ni mvivu. Usahihshaji wa CV ni muhimu sana. Tafuta mtu. Mwombe rafiki, ndugu au jamaa atakae kusaidia kusahihisha.

Kanuni 6: USIKATE TAMAA
Hii ni kanuni muhimu sana. Kama utakata tamaa baada ya MOJA au ukiwa mvivu basi hutoweza kufanikiwa lengo lako.

Jifunze mengi zaidi kwa kuangalia Video yetu ya Uandikaji wa CV kama huna Ujuzi wa kazi.