Kuna njia nyingi za kupata mtaji wa biashara yako pamoja na mifumo tofauti ya kifedha ambayo biashara yako inaweza kutumia, iawpo utahitaji mtaji. Usikatishwe tamaa na lugha ngumu inayotumiwa na taasisi za fedha. Chukua muda wako kujifunza na kumbuka: hupaswi kufanya zoezi hili peke yako! Pata ushauri mwingi uwezekanavyo.